Kufungua akaunti
- Pakua app ya YONA kutoka Google Play au App Store, au itumie kwenye browser.
- Chagua lugha: Kiswahili au English.
- Bonyeza "Anza sasa", chagua kama wewe ni mmiliki wa mradi au mtoa huduma.
- Weka jina, namba ya simu na password (angalau herufi 8).
- Weka namba ya tarakimu 6 utakayotumiwa kwa SMS ili kuthibitisha simu yako.
Kuthibitishwa (kupata alama ya Imethibitishwa)
- Nenda Akaunti → Uthibitisho.
- Kama wewe ni mtoa huduma, ongeza wasifu wako kwanza (fundi, mkandarasi, mshauri, msambazaji au msafirishaji).
- Pakia picha au PDF ya kila nyaraka inayohitajika, na weka namba yake.
- Bonyeza "Tuma kwa uthibitisho". Utapokea SMS uamuzi ukishafanyika.
- Ombi likikataliwa, utaona sababu. Rekebisha na tuma tena: nyaraka zako za awali zinabaki.
Kuomba huduma
- Kwenye ukurasa wa Nyumbani, chagua aina ya huduma au tafuta.
- Fungua mtoa huduma, angalia bei, mkoa, tathmini na kama amethibitishwa.
- Bonyeza "Tuma ombi", chagua idadi na andika ujumbe kama unahitaji.
- Mtoa huduma akikubali, lipa ada ya huduma ya YONA kwa pesa za simu.
- Kazi ikikamilika, toa tathmini ili kuwasaidia wengine.
Malipo
- Ada za YONA hulipwa kwa pesa za simu: M-Pesa, Airtel Money, Mixx by Yas au HaloPesa.
- Ukibonyeza "Lipa", utapokea ujumbe kwenye simu yako; weka PIN yako kukamilisha.
- Gharama ya kazi au bidhaa unamlipa mtoa huduma moja kwa moja kama mlivyokubaliana.
- Kila malipo yana namba ya kumbukumbu: ihifadhi kwa ajili ya ufuatiliaji.
Usalama
- Chagua watoa huduma wenye alama ya Imethibitishwa.
- Usimpe mtu yeyote PIN yako ya pesa za simu wala password yako, hata kama anadai ni wa YONA.
- Kubaliana makubaliano ya kazi kwa maandishi kabla ya kuanza.
- Ukiona jambo lisilo la kawaida, wasiliana na timu ya msaada ya YONA mara moja.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
YONA ni nini?
YONA ni jukwaa la kidijitali linalounganisha wamiliki wa miradi ya ujenzi na mafundi, wakandarasi, washauri, wasambazaji wa vifaa na wasafirishaji waliothibitishwa Tanzania.
Je, kujisajili kunalipiwa?
Hapana. Kufungua akaunti ni bure. YONA hutoza ada ndogo kwa huduma maalum kama kutangaza zabuni, kushiriki zabuni, matangazo na baada ya ombi kukubaliwa. Utaona kiasi kabla ya kulipa.
Ninalipaje?
Kwa pesa za simu: M-Pesa, Airtel Money, Mixx by Yas na HaloPesa. Unaweka PIN yako kwenye simu yako mwenyewe, hatuoni PIN yako. Gharama ya kazi yenyewe unamlipa mtoa huduma moja kwa moja.
Alama ya "Imethibitishwa" inamaanisha nini?
Inamaanisha nyaraka za mtoa huduma (kama NIDA, TIN, BRELA, CRB au ERB) zimekaguliwa na YONA, na bado ziko hai.
Nipo nje ya Dar es Salaam. Naweza kutumia YONA?
Ndiyo. YONA inafanya kazi mikoa yote ya Tanzania. Unaweza kutafuta watoa huduma kwa mkoa wako.
Nikipata tatizo na mtoa huduma nifanye nini?
Wasiliana nasi kupitia namba za msaada hapa chini au ndani ya app. Timu yetu hushughulikia malalamiko na inaweza kumsimamisha mtoa huduma asiyefuata taratibu.
Uko tayari kujenga kwa uhakika?
Jiunge na YONA leo: bure, haraka, kwa Kiswahili.